Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dada dana za Lawi, Simba vs Coastal kuna nini?

Lawi Ally Salim Msz Dada dana za Lawi, Simba vs Coastal kuna nini?

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna mambo yanafanyika kwenye soka letu yanatia kichefuchefu. Ni kama tunaishi Dunia yetu wenyewe na hatutaki kabisa kubadilika. Ni kama tumeamua kujitoa ufahamu na tunaishi kama mahayawani.

Coastal union mlikaa mezani na viongozi wa Simba na mkakubalina kufanya biashara ya mchezaji Lameck Lawi na mkakubaliana Kila kitu. Mkakubaliana gharama ya mchezaji ni Shilingi za Kitanzania Milioni 205.

Mkaweka kwenye mkataba kwamba malipo yote yanatakiwa yawe yamemalizika ifikapo tarehe 31-05-2024.

Ni kweli malipo yalipitiliza muda huo. Lakini mpaka tarehe 10 June mlikuwa tayari mmepokea malipo yenu yote Kwa mujibu wa makubaliano ya kimkataba.

Kichekesho ni pale timu Moja ya nje ya nchi inapoonyesha inamuhitaji mchezaji Lameck Lawi basi mnahangaika jinsi ya kufanya Ili muhamishe biashara kutoka Simba na mkafanye biashara na hiyo klabu kutoka nje ya nchi.

Kichekesho zaidi ni pale mnapojichanganya mnatuma email tarehe 17-06-2024 na kuamua kuweka uongo Kwa makusudi kwamba mmeituma 14-05-2024 ( Kumbukumbu za email hazijawahi kuongopa).

Na kuandika mmeamua kuvunja makubaliano Kwa kuwa Simba wameshindwa kutimiza makubaliano katika muda mliokubaliana. Muda wa makubaliano ni tarehe 31-05-2024. Barua yenu ni ya tarehe 14-05-2024.

Ina maana mliota Simba haitatimiza makubaliano? Kwenye mkataba wowote wa maazimio ya mchazaji Kwa mujibu wa kanuni za Fifa kunatakiwa kama Kuna klabu imepokea fedha kutoka klabu nyingine na inapitiliza muda wa makubaliano mnatakiwa kuiandikia kuwakumbusha wanatakiwa kulipa deni na muwaambie msipofanya hivi mpaka muda fulani tutachukua hatua zaidi.

Hilo hamkufanya. Mmesubiri mpaka mmepokea malipo yote na mkapokea bila kelele. Baada ya Sasa ya kuona Kuna klabu kutoka nje ya nchi inamuhitaji mchezaji ndio mnakuja na ngonjera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live