Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabo apotezea ushindi, aelekeza nguvu fainali

Yousuf Dabo Azammm Kocha wa Azam, Youssouph Dabo

Thu, 8 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amesema licha ya timu hiyo kupata ushindi mnono wa mabao 5-2, dhidi ya Coastal Union ila amesahau matokeo hayo, na nguvu kwa sasa anazielekeza mechi ya fainali Jumapili.

Kauli ya Dabo inajiri baada ya timu hiyo kutinga fainali ya Ngao ya Jamii na sasa inasubiri mshindi kati ya Yanga au Simba zinazocheza muda huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

"Matokeo ya sasa ni motisha nzuri kwetu wakati huu tunajipanga na mchezo wa fainali, tumeonyesha ukubwa wetu lakini inabidi kusahau yaliyopita kwa sababu bado tuna kazi kubwa iliyokuwa mbeleni kwetu," amesema.

Dabo ameongeza, amefurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na nyota wapya wa timu hiyo huku akiwataka kutobweteka na badala yake kuendelea kukipambania kikosi hicho msimu ujao.

"Ubora wa mchezaji unatokana na ushirikiano wa kila mmoja wao, ni kweli maingizo mapya yameleta kitu kipya ingawa kama ambavyo nimesema, bado tuna kazi kubwa mbeleni kwetu."

Azam inasubiri mshindi kati ya Yanga na Simba ili kujua timu itakayocheza nayo katika fainali ya Ngao ya Jamii, itakayopigwa Jumapili hii ya Agosti 11, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Mwanaspoti