Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabo akomalia mastaa Azam FC

Azam Vs Mashujaa 3 0 Dabo akomalia mastaa Azam FC

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati ligi mbalimbali duniani zikisimama kupisha michezo ya kimataifa, Kocha Mkuu wa Azam, Youssouph Dabo ameomba kwa viongozi wa timu hiyo kumpatia mechi angalau mbili za kirafiki kabla ya kukutana na Mtibwa Sugar Novemba 24, mwaka huu.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alisema baada ya ombi hilo tayari wameanza kuwasiliana na timu ndani na nje ya nchi kwa lengo la kutimiza matakwa ya kocha.

“Tumefanya mawasiliano na klabu ya Gor Mahia ya Kenya na tumekubaliana sisi ndio tutawafuata kule ila bado hatujapanga tarehe rasmi lakini naamini itakuwa kuanzia wiki ijayo, lengo ni kumtimizia mahitaji yake kama tulivyomuahidi,” alisema.

Popat aliongeza kwa sasa hali ya kikosi chao imeimarika kwa kiasi kikubwa huku akiweka wazi mzimu uliokuwa unawatesa kwa michezo ya ugenini imeondoka, hivyo viongozi wameweka jitihada kubwa kwa lengo la kuchukua ubingwa msimu huu.

“Ligi bado ni mbichi na kila timu ina nafasi ya kufanya kile ilichokikusudia, kikubwa kwetu ni kuendeleza umoja uliopo kwani bila ya hivyo hatuwezi kufikia malengo tuliyojiwekea, tunajiamini tuna wachezaji bora wanaoweza kufanikisha hilo.”

Katika michezo tisa ya Ligi Kuu Bara iliyocheza hadi sasa imeshinda sita, sare mmoja na kupoteza miwili ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 19 sawa na Simba iliyopo ya tatu ila zikitofautiana mchezo mmoja na mabao ya kufunga na kufungwa.

Chanzo: Mwanaspoti