Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabo akalia kuti kavu Azam FC

Dabo Dsc Dabo akalia kuti kavu Azam FC

Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Azam FC Youssouph Dabo amekalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo na viongozi wapo katika majadiliano ya ndani na wanaweza kutoka na maamuzi ya kuachana naye baada ya kupitia malengo aliyopewa mwanzoni mwa msimu.

Msimu wa pili sasa huu Klabu ya Azam FC inashindwa kupenya kwenye mechi za awali ili kuyaendea makundi ya CAF pamoja na kuwa na sajili kadhaa kubwa kutoka mataifa mbalimbali Afrika na Bara la Amerika.

Hadi sasa hakuna anayefahamu ugonjwa wanaougua Azam, zilizopo ni ramli tu tena chonganishi. Hii ni hasara kubwa sana kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja kama Feisal kushindwa kung'ara kwenye Michuano ya CAF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live