Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabo aanika sababu kupata ushindi mwembamba

Dabo Kocha Azam Dabo aanika sababu kupata ushindi mwembamba

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOchs wa Azam FC, Youssouph Dabo, amesema hawakupata ushindi mkubwa nyumbani kwa sababu wachezaji wake walionekana kucheza kwa presha ya kutaka kufunga mabao mapema na walipokuwa wanashindwa kufanya hivyo walikuwa wanatoka mchezoni na kushindwa kufuata maelekezo yake.

Raia huyo wa Senegal, alisema hayo baada ya timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya APR ya Rwanda kwenye mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam juzi.

Pamoja na ushindi huo kiduchu, kocha huyo alisema ana matumaini ya timu yake kusonga mbele na kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

"Nafikiri wachezaji walikuwa na hofu, kama walikuwa wanataka kufunga mabao ya haraka haraka dakika za mwanzo, lakini kila muda ulivyozidi kwenda hawapati, walikuwa wakiingiwa na presha na kushindwa kucheza kwa maelekezo.

Mapumziko niliwaambia wasiwe na haraka kwa sababu hii ni mechi ya kwanza, ya marudiano tutacheza Rwanda, hivyo watulie, watapata nafasi watafunga na hata wasipofanya hivyo (juzi), hata mechi ya mkondo wa pili wanaweza kufunga pia," alisema Dabo.

Azam ilipata ushindi huo kwa bao lililofungwa na straika raia wa Colombia, Jhonier Blanco dakika ya 56 kwa mkwaju wa penalti, baada ya Feisal Salum kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

"Nimeifutilia APR ni timu ambayo huwa hairuhusu mabao kirahisi, mabeki wake wapo vizuri, kwa maana hiyo inabidi tujipange vema katika mechi ya marudiano.

"Tunakwenda kucheza nchini Rwanda, tuna uhakika wa kushinda kwa sababu tuna kikosi kizuri cha kuweza kushinda pia ugenini," alisema kocha huyo.

Kocha Mkuu wa APR, Mserbia Darko Novic, alisema ana wasiwasi kama ilikuwa penalti sahihi, lakini akawapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuwazuia Azam.

"Tumecheza na timu nzuri, tumepoteza kwa bao 1-0, kwa hiyo tunajipanga kwa mchezo ujao, ila kuna nafasi tumepoteza ambazo zingeweza kufanya mchezo uishe kwa sare," alisema Darko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live