Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabi yampa mbinu kocha Vital’O dhidi ya Yanga CAFCL

Vital O' Dabi yampa mbinu kocha Vital’O dhidi ya Yanga CAFCL

Sun, 11 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Vital ‘O ya Burundi, Sahabo Parris amesema ameutazama mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga na ameutumia kuisoma Yanga na kujua uimara wao, huku akiamini hadi timu hizo zitakapokutana atakuwa ameshapata mbinu bora za kuwakabili.

Vital’O itakutana na Yanga katika mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika Agosti 17 na kurudiana Agosti 24, mechi zote zikichezwa jijini Dar es Salaam nadhidi ya Pamba Jiji katika Tamasha la Pamba Day.

Akizungumza jijini Mwanza, Parris alisema ameisoma Yanga na kujua wakishambulia lango la mpinzani wanakuwa na kasi ya ajabu lakini mchezo dhidi ya Pamba utawasaidia kimbinu na kuboresha upungufu wao kabla ya kuivaa Yanga wikendi ijayo.

“Juzi nimeona mechi ya Yanga dhidi ya Simba tumefuatilia jinsi wanavyocheza hasa wakiendea lango la wapinzani, wana kasi kubwa hivyo tutajitahidi tucheze nao tupate ushindi mechi ya kwanza na ya marudiano tuzuie na kulinda ushindi wetu ili tusonge mbele,” alisema Parris na kuongeza;

“Mechi ya Pamba sio kipimo tosha, lakini hatutaudharau mchezo utatusaidia kwa sababu nao wana timu nzuri na wamesajili vizuri, tumeshajipima na kucheza mechi nyingine nyumbani, lakini tumekosa timu za kucheza mechi za kirafiki za kimataifa kwahiyo hii ya Pamba inatusaidia.”

Akizungumzia changamoto ya nchi ya Burundi kukosa uwanja unaokidhi vigezo vya kimataifa na kulazimika kucheza mechi zao Tanzania, Parris alisema ni mtihani lakini hawaogopi kwani wamejiandaa kucheza popote, na ni afadhali kutumia Uwanja wa Azam kuliko Benjamin Mkapa ambao ni ngumu kuwakabili wenyeji wao.

Nahodha wa kikosi hicho, Hussein Ndayishimiye, alisema watautumia mchezo wa Pamba Jiji vizuri bila kudharau chochote ambapo wanauchukulia kama mchezo baina ya mataifa mawili hivyo utawasaidia kwenye mechi zao zijazo ukiwemo dhidi ya Yanga.

“Tuko vizuri tumefanya mazoezi tangu nyumbani mpaka hapa tumekamilika, hakuna majeraha, kwetu wachezaji huu ni ushindani wa nchi kwa nchi, ni mchezo mkubwa tuna imani tutashinda kwa sababu benchi la ufundi limetupatia mbinu bora,” alisema Ndayishimiye na kuongeza;

“Tumecheza mechi nyingi nyumbani hii mechi (dhidi ya Pamba) itatusaidia kujua namna Watanzania wanavyocheza, wachezaji tuna maandalizi ya kutosha mwalimu ametupa mbinu nzuri, mashabiki watapata burudani na kutoka uwanjani wamefurahi.”

Chanzo: Mwanaspoti