Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabi ya Yanga na Mamelodi yapewa jina maalum na CAF

Maxi Yangaa (29).jpeg Dabi ya Yanga na Mamelodi yapewa jina maalum na CAF

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi ya Wananchi, Young Africans Sc dhidi ya Mamelodi Sundowns almaarufu 'Masandawana' imepewa jina rasmi na wadhamini wa CAF (Total Energies) la 'SADC Derby'.

Kwa mujibu wa CAF, hakuna mechi kubwa nyingine iliyowahi kutokea kama hii ukanda huu wa nchi za Kusini mwa Ikweta au Jangwa la Sahara (Ukanda huu wa Jumuiya ya SADC)

Rangi ya njano ni rangi maalum kwa jezi na bendera ya timu zao na hata mataifa yao yote mawili.

Jumuiya ya SADC inajulikana kama The Southern African Development Community kifupi chake (SADC) kwa maana ni Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Kusini wa Bara la Afrika.

SADC ilianzishwa Mwaka 17/08/1992 Ikiwa makao Makuu yake Nchini Botswana Mpaka sasa ina Muunganiko wa nchi 16.

01 Zambia

02 Angola

03 Tanzania

04 Africa Kusini

05 Comoro

06 DR Congo

07 Malawi

08 Namibia

09 Zimbabwe

10 Mauritius

11 Lesotho

12 Madagasca

13 Seychelles

14 Eswatine

15 Mozambique

16 Botswana

Katika Ukanda huu wa SADC Una utajiri wa timu tano zikiwakilisha Simba,Yanga Mamelodi Sundowns na Petro De Luanda nchini Angola pamoja na TP Mazembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live