Ni kama kutimia tu kwa yaliyotarajiwa! Kulikuwa na nafasi kubwa kwa Yanga kushinda mchezo kwa Perfomance yao ya siku za karibuni.
Wapo kwenye kiwango kizuri zaidi na sasa wamemla Mnyama nje ndani. Moja ya mechi nzuri sana tu kiuchezaji.
Yanga wanapoamua kukukabia juu wanakupa kigugumizi. Wanafika Kwa haraka kulazimisha ukosee. Walipata goli la kwanza kwa msingi huo na kipindi cha pili walionekana kukosa umakini na kupoteza nafasi kadhaa.
Simba walizidiwa kipindi cha kwanza karibu chote. Kipindi cha pili walikuwa bora... Waliamua kushambulia na kuwasogelea Yanga bila uoga. Walipata goli zuri sana la Fredy akitumia vyema uzembe wa mabeki wa Yanga.
Aziz KI ni pesa ile Yanga wana urahisi mwingi wakiwa naye kiwanjani. Anajua sana kulinda mpira anapouhitaji na anajua sana kuamua matukio kadhaa tu. Ndiye Man of the Match wangu leo.
Well played Hussein Kazi... Kuna mechi zinahitaji utimize basics tu... Kosa lake moja halifuti mazuri yake mengi mchezoni. Kiwango bora sana hasa ukikumbuka lilikuwa badiliko la lazima✍️
Napenda uchezaji wa Aucho! Hawazi kufanya mambo mengi zaidi ya kupasia, kufungua na kurudisha umiliki wa mpira✅ Anaweka wepesi sana kwa walinzi wake na leo Mudathir alikuwa chini ya ubora wake na Aucho alifanya kazi nyingi kuziba hayo.
Kibu Denis anahangaika sana kule mbele Siku akipata usahihi wa matendo ni moja ya wachezaji wazuri... Shida yake ni kutokujua anafanya nini akiwa wapi. Ana heka heka za hatari.
Mechi nzuri Dickson Job... Ni mchezaji mwenye nidhamu ya eneo lake, utulivu anapofanya maamuzi na timing sahihi sana kwenye matendo yake!
Well played Chama Clatous.
Kwenye zile dakika za Magharibi ya roho chochote kingeweza kutokea. Wananchi kwenye kilele cha furaha... Wamerudia walichokifanya 2015/16.
Arajiga mhh????
FT' Yanga SC 2 vs 1 Simba SC
Wasalaam!