Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dabi ya Kariakoo: Timu bora imeshinda mechi ngumu

Aziz Ki Simba Yanga Aziz Ki

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu bora imeshinda mechi, ilikuwa game ya nguvu, kasi na mbinu nzito kwa kila upande. Kwenye mpira wa miguu tunasisitiza kitu kinachoitwa many mistakes ukikifanya sana unahatarisha uvunaji wa alama 3 na kushinda mechi, Yanga walifanya nini?

1: Kukabia juu sana ili kutompa spaces kubwa za kupitisha pass nyingi Simba kutoka safu ya Ulinzi hadi safu ya Ushambuliaji, repeatedly walifanikiwa sana.

2: Kucheza man to man ili kumfanya Simba asiweze kutafuna distance yao kuanzia kwenye mistari yote mitatu, na kunufaika na pass zilizopigwa vibaya hasa Kiungo cha Simba .

3: Ile counter pressing walizokuwa wakizifanya Nzengeli, Mudathir na Aucho ziliwaweka hai sana Yanga wakipoteza mpira, halafu build up ya haraka sana hadi na langoni kwa Simba.... Bang! Chuma mbili.

Simba walikuwa wakikaba kuanzia katikati, na zile dakika 15 za mwanzo waliukamata mchezo lakini finishing yao ilikuwa butu sana, ukilinganisha na nafasi kadhaa walizotengeneza.

Kanoute, Chama walipaswa kuwa compact na kuweka mpira wavuni, nini walichofanya kipindi cha pili?

1: Kuzuia njia za mpira za Yanga ambapo Sarr, Chama, Mzamiru walifanikiwa sana na kuifanya shape ya timu kurudi kwenye muhimili mzuri sana ,timu ilitulia

2: Kufanya high pressing kwa kasi zaidi, kitendo kilichowapa shida sana Aucho, Mudathir, Nzengeli kwa maingizo mapya (Freddy, Miquissone, Jobe).

3: Yes, kuna move walifanya Simba ilikuwa super sana (Chama na Freddy) walikuwa bora sana hata rotations yao kiwanjani... Mara wakapata goli moja.

NOTE

1: KI Aziz anajua sana kukaa na mpira (ball possession) ya hali ya juu sana, amewapika sana viungo wa Simba.

2: Sarr amemwaga jasho la kutosha, kuna kiungo mzuri ndani yake.

3: Mzize kwa zile runs zake za hatari sana, kutunza mali alikuwa na game nzuri sana

4: Energy na strength ya Kibu

5: Nafikiri Simba itakuwa imefahamu kuwa Yanga ni bora zaidi kuliko wao msimu huu, mechi mbili zote alama 6 kwenye msimamo daah quality.

6: Guedé ni hatari kwenye finishing, amewapa ubusy sana mabeki wa Simba aiseee anajua kufunga.

7: Yanga ni wazi kuwa Yanga wachezaji wao wametimiza majukumu yao ipasavyo, ubingwa uleee .!

FT: Yanga 2-1 Simba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live