Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Da Cruz atambulishwa Brazil

Fa Cruz Ms.jpeg Da Cruz atambulishwa Brazil

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa mshambuliaji wa Singida Big Stars, Peterson Da Cruz ‘Peu’ ametambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Clube Nautico Marcilio Dias inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini Brazil ‘Serie D’ mara baada ya kurudi nyumbani kwao akitokea Tanzania.

Awali Mwanaspoti liliripoti juu ya shikinizo la familia yake ambayo ilihitaji kuwa naye karibu hivyo viongozi wa Singida BS hawakuwa na budi zaidi ya kutoa ruhusa kwa mchezaji huyo ili akatatue changamoto hiyo.

Lakini baadaye ikabidi waachane na mchezaji huyo ambaye alifunga bao moja Ligi Kuu Bara.

Siku chache baada ya kuondoka nchini, Peu amekuwa ingizo jipya kwenye kikosi cha Clube Nautico Marcilio Dias ambacho kinapambana kuhakikisha kinapanda daraja, nyota huyo anaamini kwamba hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kurejea kwao.

“Napenda kuishukuru klabu (Singida BS) kwa kuamini kazi yangu, na mashabiki kwa upendo wote ambao wamenionesha kwa miezi yote nilipokuwa naitumikia. Kucheza soka barani Afrika umekuwa ni uzoefu wa kipekee ambao nitaendelea kuishi nao milele.”

“Lakini mwisho wa safari moja ni mwanzo wa nyingine, nimerudi nyumbani na nitakuwa hapa hadi pale ambapo itakuwa mwisho na mwanzo wa nyakati nyingine,” alisema.

Taarifa rasmi ya utambulisho wake kwenye klabu hiyo ilisema: “Straika Peu da Cruz, mzaliwa wa Navegantes, mwenye umri wa miaka 29, anarudi kwa Giant kuvaa rangi za pete nyekundu....Katika wasifu, Peu analeta uzoefu...”

Chanzo: Mwanaspoti