Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DTB inaingia sokoni dirisha dogo

DTB FC Kikosi cha DTB kufanya usajili Januari

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: Mwanaspoti

DTB FC inaonekana kunogewa na kazi inayofanywa na mastaa wake waliowahi kucheza katika Ligi Kuu hasa kwenye timu kubwa na sasa imepanga kuongeza wengine katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao.

Mratibu wa timu hiyo, Muhibu Kanu ameliambia Mwanaspoti kuwa kitendo cha kutopoteza mchezo wowote wa Ligi Daraja la Kwanza hadi sasa ni ishara tosha kuwa uzoefu na ubora wa nyota waliowahi kutamba Ligi Kuu umekuwa na faida kwao hivyo wataongeza wengine ili kumalizia kazi ambayo imeanza kufanyika

“Timu hadi sasa ipo katika mwelekeo mzuri na kama mnavoona tunaongoza msimamo wa ligi huku tukiwa hatujapoteza mchezo wowote na hii inathibitisha kwamba wachezaji wetu wana viwango vizuri na uzoefu wao umeendelea kutusaidia.

Katika dirisha dogo tutaongeza baadhi ya wachezaji nyota wa timu za Ligi Kuu ambao tunaamini wataongeza nguvu kwa waliopo ili tuweze kutimiza malengo yetu ya kupanda daraja. Hawa waliopo ni wazuri lakini nao wanatakiwa kuongezewa nguvu na kuwafanya wapinzani wasitukariri,” amesema Kanu.

Nyota waliowahi kutamba Ligi Kuu ambao wapo kwenye kikosi cha DTB ni Amissi Tambwe, David Mwantika, Issa Makamba, James Msuva, Nicholas Gyan, Yusuf Mlipili, Emmanuel Mseja, Owen Chaima, Juma Abdul, Saad Kipanga, Tafadzwa Kutinyu na Shaban Majaliwa.

Timu hiyo katika mechi sita ilizocheza hadi sasa, imeibuka na ushindi mara nne na kutoka sare katika michezo miwili, imefunga jumla ya mabao 11 na imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara nne tu.

Katika mabao 11 ambayo imefunga, matano yamepachikwa na nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Amissi Tambwe.

Chanzo: Mwanaspoti