Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DROOCAFCL: Hii hapa faida Simba kupewa Al Ahly

Droo Full DROOCAFCL: Hii hapa faida Simba kupewa Al Ahly

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CAF wametangaza droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa ambapo Simba SC, wamepangwa na Al Ahly na kwa mujibu wa kanuni, Simba ataanzia nyumbani na kumalizia ugenini.

Faida ya Simba kuchezwa na Al Ahly, wanaifahamu vizuri kwani ametoka kucheza nao kwenye kombe la African Footbal, Simba alipata sare ya 2-2 nyumbani na ugenini akatoka 1-1 hivyo Al Ahly kuvuka kwa faida ya goli la ugenini.

Kama hiyo haitoshi, Simba kwa siku za karibuni, amekuwa akipata matokeo kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Mechi ya kwanza ya nyumbani itapigwa kati ya 29-31, Marchi na za kurudiana baadaye Apili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live