Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DONDOO ZA SOKA: Greenwood kubaki mazima Hispania

Mason Greenwood Brace Mason Greenwood

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Sociedad wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili Mason Greenwood mara baada ya msimu wake wa mkopo Getafe utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu.

Valencia ni miongoni mwa timu za LaLiga zinazomtazama fowadi huyo aliyeko kwa mkopo Man United.

Bayern Munich wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa angalau vilabu viwili vya Premier League mwezi Januari katika mbio za kumsajili nyota wa Fulham Joao Palhinha.

Bayern wanatarajiwa kurekebisha mbinu zao baada ya ofa yao ya pauni milioni 60 kuporomoka msimu wa joto.

Manchester City na Liverpool wamedhamiria kumsajili Florian Wirtz wa Bayer Leverkusen. Miamba hao wa Ligi ya Premia bado wana matumaini ya kumenyana na Bayern Munich licha ya timu hiyo ya Bundesliga kusalia ikipewa nafasi kubwa ya kumsajili nyota huyo wa

Newcastle na Tottenham wanafikiria kumnunua winga wa Juventus Samuel Iling-Junior, 20.

Timu hiyo ya Serie A iko tayari kufikiria ofa za kudumu kwa Iling-Junior kutokana na mkataba wake kuisha mwaka wa 2025

Juventus wameweka bei ya pauni milioni 34 kwa ajili ya Kenan Yildiz anayewindwa na Arsenal.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 amecheza mechi tano kwenye kikosi cha kwanza cha Kibibi Kazee cha Turin na tayari ameshaichezea timu ya taifa ya Uturuki mechi tatu.

Liverpool wanamfuatilia beki wa kati wa Sao Paulo Lucas Beraldo. Klabu hiyo ya Brazil ilikataa ofa kutoka kwa Wolves katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Arsenal wanajiandaa kumnunua kiungo wa Aston Villa Douglas Luiz lakini wanatarajia kuwa dili litakuwa gumu huku kikosi cha Unai Emery kikitaka zaidi ya pauni milioni 60 ili kufikiria dili hilo.

FC Bayern Munich itakubali kufanya mazungumzo na Real Madrid juu ya uhamisho wa Alphonso Davis kama sehemu ya kubadilishana wachezaji.

Bayern Munich wanamtaka Rodrigo katika dili hilo.

Atletico Madrid wanataka kumsajili beki wa klabu ya Lille Tiago Djalo katika dirisha dogo la uhamisho la mwenzi January.

Ferran Torres anaweza kuondoka FC Barcelona. watu wake wa karibu hawana uhusiano mzuri na makocha wa Barça na ujio wa Vitor Roque ni sababu nyingine pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live