Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DFB yasaini Mkataba wa Euro Milioni 100 na Nike

DFB Soccer DFB yasaini Mkataba wa Euro Milioni 100 na Nike

Sat, 23 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uamuzi wa shirikisho la soka Ujerumani kuachana na Kampuni ya Adidas kama msambazaji wake wa jezi ulizua taharuki mjini Berlin siku ya Ijumaa, huku Waziri wa Uchumi akilaani kubadili Kampuni kubwa na kusaini mkataba na Nike ni kama ukosefu wa uzalendo.

DFB siku ya Alhamisi ilisema itasitisha ushirikiano wake wa miongo kadhaa na Adidas, ikichagua Nike kama msambazaji wake mpya kuanzia mwaka wa 2027.

Timu za taifa za Ujerumani zilikuwa zinavaa jezi za Adidas tangu miaka ya 1950, tangazo hilo la kushitukiza likiwa limekuja miezi michache tu kabla ya michuano ya kandanda ya Ulaya kwa upande wa wanaume kuanza kutimua vumbi nchini Ujerumani mwezi Juni.

Mkataba na Nike, ambao utaendelea hadi 2034 ambao thamani yake ni takribani euro milioni 100 (dola milioni 108) kwa mwaka mara mbili ya thamani ya mkataba wa Adidas.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live