Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Curtois alia na safu ya ulinzi Real Madrid

Thibaut Courtois Kw79b27bsone1uviearp1rb6z Golikipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa Real Madrid Thibaut Courtois ameonyesha kusikitishwa kwake na Real Madrid hasa kwa upande wa walinzi wa timu hiyo kwa kuruhusu mabao mengi kwa urahisi kabisa na kusababisha kupoteza mchezo wao wa kwanza kwenye Laliga msimu huu kwa mabao 3-2 dhidi ya Rayo Vallecano.

Courtois amelalamika jambo hilo huku akiona kama hakuna dalili ya kuchukua tuzo ya golikipa bora kutokana na timu yake kuruhusu mabao mengi na mpaka sasa ndani ya michezo 13 amepata Clean Sheets mbili tu.

Golikipa huyo amesema kuwa;

“Rayo wana msimu mzuri, tulijua itakuwa ngumu, na hatukuweza kutekeleza jukumu hilo katika kipindi cha kwanza, tuliruhusu mabao mengi ya kijinga kutokana na makosa au kutokuwa na asilimia 100 kwenye mechi.”

Kwa kuwa na michezo mingi, inaweza kuwa kawaida kwamba wamechoka, huku akigusia kwa kusema kuwa sare dhidi ya Girona ilikuwa bahati mbaya zaidi na jana haikuwa siku yao bora na Rayo Vallecano walicheza vizuri.

Wakati Courtois alikataa kumkosoa mwamuzi Juan Martinez Munuera, mchezaji mwenzake wa Madrid Lucas Vazquez alihoji kwa nini VAR na maafisa hawakuwa “wakali” katika michezo mingine msimu huu.

Na mchezaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa mchezo ulikuwa mgumu, walisonga mbele kwa haraka sana na ingawa waliweza kusawazisha tena na hilo liliwaumiza zaidi. Rayo ni timu ngumu ambayo jana ilikuwa nzuri sana.

Baada ya kupoteza mchezo huo kwa mara ya kwanza Madrid inashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa nyuma kwa pointi 2 dhidi ya vinara wa Laliga Barcelona na itawakaribisha Cadiz siku ya Alhamisi katika mchezo wao wa mwisho kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live