Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cunha awapa mzuka Man United

Skysports Matheus Cunha Wolves 6005909 Matheus Cunha

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imeripotiwa kuongezewa mzuka kwenye harakati zao za kumsajili fowadi wa Wolves, Matheus Cunha.

Man United ipo sokoni kusaka straika mpya baada ya Anthony Martial kuachana na timu hiyo wakati mkataba wake ulipofika ukomo mwishoni mwa mwezi Juni.

Kocha mkuu wa Man United, Erik ten Hag, anaye mshambuliaji Marcus Rashford kwenye kikosi chake ili kushindania nafasi na Rasmus Hojlund, lakini Mdachi huyo amekuwa akifikiria kuwaanzisha pamoja kwenye kikosi chake.

Kutokana na hilo, Man United sasa inahitaji straika mwingine kwenye dirisha hili, ambaye atakuwa anatokea benchi wakati wawili hao watakaoanzishwa. Man United inaamini pia itaweza kupata huduma ya mshambuliaji huyo wa Kibrazili, Cunha kwa dau la chini.

Wakati akiwa kwao Brazil, mshambuliaji Cunha alisema anafurahia kuwapo Molineux kutokana na kile alichokifanya kwenye msimu wa 2023-24.

Hata hivyo, staa huyo mwenye umri wa miaka 25, ameonyesha wazi yupo tayari kutimkia Man United, endapo kama miamba hiyo ya Old Trafford itakuwa siriazi kwenye kunasa huduma yake.

Cunha alisema: “Unajua hii ni heshima kubwa kuhusishwa na Manchester United. Ni moja ya klabu kubwa duniani. Lakini, nina furaha Wolves. Kama nitakuwa na bahati, nitacheza kwa kiwango bora msimu ujao, lakini dirisha lipo wazi na huwezi kujua kitakachotokea.”

Wolves inajiamini kwamba itaendelea kubaki na Cunha kwa sababu mkataba wake umebakiza miaka mitatu.

Wolves ililipa Pauni 44 milioni kunasa saini ya Cunha na Man United inaamini itanasa saini ya mshambuliaji huyo wa dili lisilozidi Pauni 60 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti