Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Crouch amshangaa Ronaldo De Lima

Crouch Ronaldo Crouch amshangaa Ronaldo De Lima

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Peter Crouch amefichua kukutana kwake na Ronaldo Nazario alipokuwa likizoni nchini Uhispania.

Mshambulizi huyo wa zamani wa Liverpool na Tottenham Hotspur, ambaye anatambulika kama wanasoka wengi duniani kote, alifadhaika Mbrazili huyo alipokosa kujua yeye ni nani.

"Nilikutana na Ronaldo (De Lima) mara moja nilipokuwa likizo kule Ibiza. Alikuwa amezungukwa na warembo ufukweni na chupa za bia kibao tu. Ilikuwa kila akimaliza kinywaji basi mrembo mmojawapo anampatia chupa nyingine.

"Niliona huo ndio muda sahihi wa kupiga naye picha, nikajisogeza pale nikajua hata atasema 'Ooh.. Crouch'... lakini haikuwa hivyo. Nilipiga picha yangu nikaondoka. Hata hakujua mimi ni nani na hakujua kama mimi pia ni mchezaji wa mpira," amesema Crouch.

Unamkumbuka huyu jamaa, Peter Crouch kwa lipi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live