Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Crouch: Sitashangaa Kane akiondoka Spurs

Kane And Conte Mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane akiteta jambo na Conte

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa soka Peter Crouch hakuona maana ya Tottenham kushikiri michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu huu baada ya kung'olewa na AC Milan.

Spurs imetolewa kwa faida ya bao la AC Milan lililopatikana kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 bora ya Ligi Mabingwa Ulaya, aidha katika mechi ya marudiano ulimalizika timu hizo zikitoka suluhu.

Spurs ilishindwa kutengeneza nafasi kwenye mchezo huo wakiwa pungufu baada ya beki wao kisiki Cristian Romero kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Kwasasa Tottenham inapambana kwenye ligi ifuzu michuano ijayo ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu ujao, na imejikita nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, huku wakiwa na matumaini ya kupata ushindi kwenye mechi zinazofuata dhidi ya Liverpool na Newcastle.

Lakini nyota huyo wa zamani wa Tottenham, bado akajiuliza kwamba haoni maana ya timu hiyo kushiriki michuano kwasababu wamezingua, hatashangaa Harry kane akiamua kuondoka msimu ukimalizika.

"Sijui kwanini hata sielewi, timu iliyopo nafasi ya 'Top Four' inacheza kwa kiwango hiki kwenye michuano mikubwa kama hii, mashabiki wanataka makombe, kupumzisha wachezaji kwaajili ya mechi za Kombe la FA halafu baadaye wanatolewa, sidhani kama nahodha wao ataendelea kuwepo hapa" alisema Croach

Taarifa ziliripoti Man United imeanza kumnyemelea straika huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye mkataba wake wa sasa utamalizika itakapofika mwaka 2024, vile vile kuna mazungumzo ya siri yanasemwa kamba Antonio Conte naye huenda akaondoka kama mambo yataendelea kuwa hovyo.

Kane akaongezezea kwa kusema " Kane atasubiria mambo ya mpito kwa muda gani? sidhani kama atachukuwa muda mrefu baada ya hapa, nafikiri watu hawatamwekea kinyongo endapo ataondoka siku za usoni,"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: