Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Croatia wakabiliwa na shutuma za unyanyasaji

Borjan Canada Croatia wakabiliwa na shutuma za unyanyasaji

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Croatia wamekabiliwa na hatua za kinidhamu baada ya kipa wa Canada Milan Borjan kulengwa na mashabiki wakati wa mechi yao ya Kombe la Dunia wiki iliyopita.

FIFA imefungua kesi Jumanne “kutokana na tabia ya mashabiki wa Croatia. Borjan ni Mserbia wa kabila ambaye alizaliwa Knin huko Crotia lakini alikimbia na familia yake hadi Belgrade mwaka wa 1995 wakati wa oparesheni ya mashambulizi ya Croatia katika vita vyake vya uhuru.

Baadaye alihamia Canada, nchi ambayo anaiwakilisha katika ngazi ya Kimataifa, lakini ametumia muda mwingi wa klabu yake nchini Serbia, ambako sasa anachezea Red Star Belgrade.

Wakati wa ushindi wa 4-1 wa Croatia dhidi ya Canada, Borjan alipewa bendera kwenye viwanja iliyosomeka “Knin ’95 huku akiimbiwa nyimbo za kuudhi ambazo ziliripotiwa kulenga mwelekeo wake.

Baada ya mchezo huo Borjan alisema kuwa; “Sina la kusema juu ya hilo, nilisikia walipiga kelele na kunitukana.”

Hiyo inaonyesha kwamba wao ni watu wa kizamani na wanapaswa kujishughulisha wenyewe na familia zao kwasababu ni wazi wana changanyikiwa kwahivyo wanakuja na kuibua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live