Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cristiano Ronaldo ashinda Tuzo ya Maradona

Cristiano Ronaldo Al Nassr Saudia Cristiano Ronaldo.

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Al Nassr FC ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo ameshinda Tuzo ya Maradona kutoka Globe Soccer kama mfungaji bora wa mwaka 2023 akiwa na magoli 54.

Ronaldo anakuwa mchezaji wa pili kutwaa tuzo hiyo baada ya Mpoland Robert Lewandowski aliyetwaa mnamo 2022.

Ronaldo (38) raia wa Ureno ni mchezaji wa kwanza kutoka Ligi ya Saudi Arabia kutwaa tuzo hiyo.

RONALDO - 2023:-

Amepokea tuzo ya mfungaji bora Duniani kwa mwaka 2023 kutoka Shirikisho la Kimataifa la Historia ya mpira wa miguu na takwimu Duniani (IFFHS).

Amepokea tuzo ya Maradona kama mfungaji bora Duniani kwa mwaka 2023 kutoka #GlobeSoccer.

Amepokea tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Desemba 2023 kutoka #SaudiProLeague. Mwezi ujao siku kama ya leo anatimiza miaka 39.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live