Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cristiano Ronaldo asema Glazers hawaijali Manchester United

B7cb123a A27e 4279 Ae25 59379e6047c0 Cristiano Ronaldo asema Glazers hawaijali Manchester United

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Mshambulizi wa Manchester United Cristiano Ronaldo anasema wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazer, "hawaijali klabu" kwenye upande wa michezo.

Ronaldo aligonga vichwa vya habari baada ya kuiambia Talk TV anahisi "amesalitiwa" na klabu - na sehemu nyingine ya mahojiano hayo ilitolewa Jumatatu usiku.

"Manchester ni klabu ya masoko - wanapata pesa kutokana na masoko," alisema.

"Itakuwa vigumu kwa Manchester kuwa kinara wa mchezo katika miaka miwili au mitatu ijayo."

'Neville na Rooney sio marafiki zangu'

Katika sehemu ya Jumapili ya mahojiano, Ronaldo aliulizwa kama alikuwa na hasira kwamba alikosolewa na mchezaji mwenzake wa zamani wa United Wayne Rooney - ambaye sasa anaiongoza DC United.

Ronaldo alisema: "Pengine, kwa sababu alimaliza soka akiwa miaka ya thelathini. Mimi bado nacheza kwa kiwango cha juu. Sitasema kwamba ninaonekana bora kuliko yeye, ambayo ni kweli, lakini ... ."

Chanzo: Bbc