Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cristiano Ronaldo ajiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia

Cristiano Ronaldo Ajiunga Na Al Nassr Ya Saudi Arabia.png Cristiano Ronaldo ajiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia

Sat, 31 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Cristiano Ronaldo amejiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia kwa mkataba utakaodumu hadi 2025.

Nahodha huyo wa Ureno ni mchezaji huru baada ya kuondoka Manchester United kufuatia mahojiano yenye utata ambapo aliikosoa klabu hiyo.

Ronaldo anaripotiwa kupokea mshahara mkubwa zaidi wa kandanda katika historia wa zaidi ya £177m kwa mwaka.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 anasema "anatamani kupata uzoefu wa ligi mpya ya soka katika nchi tofauti".

Ronaldo aliongeza: "Nina bahati kwamba nimeshinda kila kitu nilichodhamiria kushinda katika soka ya Ulaya na ninahisi sasa kwamba huu ni wakati mwafaka wa kubadilishana uzoefu wangu huko Asia."

Al Nassr - mabingwa mara tisa wa Saudi Pro League - walielezea usajili huo kama "historia inayoundwa".

Klabu hiyo ilisema "itahamasisha ligi yetu, taifa na vizazi vijavyo, wavulana na wasichana kuwa bora zaidi ".

Katika majira ya joto, Ronaldo alikataa mkataba wa £305m kujiunga na timu nyingine ya Saudi - Al Hilal - kwa sababu alikuwa ameridhika kusalia Man United

Chanzo: Bbc