Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cristiano Ronaldo Jr anatumia Tsh milioni 100 kwa wiki

Dsc Ronaldo Jr Cristiano Ronaldo Jr anatumia Tsh milioni 100 kwa wiki

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahojiano ya supastaa wa Al-Nassr ya Saudi Arabia na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo alipohojiwa na "Will to Act" amelalamikia gharama za mwanae Cristiano Ronaldo Jr kuwa kubwa yamesambaa mitandaoni.

"Anatumia zaidi ya euro 35,000 (Tsh milioni 100.55) kwa wiki kwa kunyoa nywele, nguo, migahawa na marafiki zake wa kike. Najua yeye ni mdogo na anataka kila kitu, lakini nadhani ni pesa nyingi sana kwa mtoto wa umri wake," alisema mwanasoka huyo maarufu.

Mtoto huyo ana umri wa miaka 14, amekuwa akisoma katika academy za soka za vilabu ambako baba yake anacheza.

"Sasa ninampa tu euro 13,000 (Tsh milioni 37.35) kwa wiki, lakini Georgina bado anafikiri ni nyingi sana. Anazitumia zote kwenye migahawa, kwenda nje na mambo mengine ambayo hayana manufaa," nyota huyo wa soka aliongeza.

Cristiano Ronaldo Jr alizaliwa Juni 2010 huko San Diego, California na bado haijajulikana mama yake ni nani. Mwanasoka huyo ana jumla ya watoto watano. Wawili na mchumba wake, Georgina Rodriguez na wengine watatu kutoka kwa mahusiano ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live