Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cr7 azidi kukimbiza YouTube

CR YOU TUBE Cr7 azidi kukimbiza YouTube

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa wa Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amefungua chaneli yake ya mtandao wa YouTube na kuweka rekodi ya kufikisha wafuasi milioni moja ndani ya saa moja, juzi Jumatano.

Ronaldo, ambaye anatimiza umri wa miaka 40 msimu huu, alizindua chaneli yake hiyo kwa video ya dakika moja ikielezea maudhui yatakayowekwa.

Fundi huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid ameweka wazi chaneli hiyo itakuwa inaweka maudhui ya nyuma ya pazia, pamoja na video zake akikabiliana na changamoto, akicheza michezo na mpenzi wake Georgina Rodriguez na kufanya mazoezi.

Vile vile, Ronaldo aliweka rekodi nyingine ya chaneli yake kufikisha wafuasi milioni 14.2 ndani ya saa 24 pekee.

Rekodi ya awali chaneli ambayo ilifikisha wafuasi milioni 10 ilichukua siku saba.

Pamoja na kuvunja rekodi, Ronaldo amezua tafrani kwa video zake chache aliweka katika chaneli hiyo.

Video hiyo ilikuwa inahusu maswali yake ya Mr & Mrs aliyokuwa akishirikiana yeye na Georgina Rodriguez ambayo yalizua tetesi za wawili hao kuwa huenda wamefunga ndoa.

Licha ya kwamba inajulikana hawajafunga pingu za maisha, Ronaldo alisikika akimwita mrembo huyo “mke” na vidoleni walionekana amevaa pete.

Ndani ya saa 24 tangu alipoizindua Ronaldo tayari alikuwa amepakia video 19 kwenye chaneli hiyo.

Na nyota huyo ameahidi kutoa ufahamu juu ya familia yake, elimu na biashara, pamoja na kuhoji wageni maarufu.

Chanzo: Mwanaspoti