Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Covid-19 yazidi kumtesa Kimmich

Kimmich Joshua Kimmich

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiraka wa Bayern Munich Joshua Kimmich atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu kutokana na kupata shida ya mapafu inayochagizwa na matokeo ya virusi vya Covid-19.

Kimmich, 26, ambaye aliweka wazi kuwa hakupata chanjo ya Corona mwezi Octoba wakati wachezaji wengine wakipata, alikutwa na maambukizi ya Corona mwezi uliopita.

Muda wa kujitenga mwenyewe ulimalizika Jumatano ya Disemba 5 lakini kutokana na kadhia hiyo atalazimika kuwa nje ya kikosi cha Bavarian mpaka mwanzoni mwa mwaka 2022.

Akizungumzia hali yake Kimmich alisema anajisikia vizuri ingawa alikiri kuwa hajapata ruhusa ya kuanza kuufanyika kazi ngumu mwili (kukimbia) kutokana na kuwa na shida kwenye mapafu.

Kimmich tayari amekosa mechi tatu za Ligi Ausburg, Arminia Bielefeld, Borrusia Dortmund pamoja na mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kyiv na Fc Barcelona, hata hivyo atakosa mechi nyingine dhidi ya Mainz, Stuttgart na Wolfsburg kabla ya Bundesliga kuingia kwenye mapumziko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live