Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Covid- 19 yaivuruga EPL, Vilabu kukutana jumatatu kujadili nini cha kufanya

Klopp Pic Data Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp hakubaliani na suala la kusitishwa kwa mechi

Sat, 18 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu za Ligi Kuu England (EPL) zitakutana Jumatatu kujadili mzozo unaoendelea unaozingira janga la virusi vya corona.

Huku mechi tisa zikiahirishwa katika kipindi cha wiki moja iliyopota, ikiwa ni pamoja mechi tano za wikendi hii mechi zilizokuwa kwenye ratiba, klabu zinataka muda wa kujadili nini la kufanya.

Mameneja na manahodha pia watafanya mikutano yao.

Meneja wa Aston Villa Steven Gerrard alisema kuwa anamatumaini mkutano huo utaweka "mambo wazi " kuhusiana na "hofu kubwa zilizopo na maswali ambayo hayajajibiwa''.

Wakati huo huo, Mkuu wa Primia Ligi Richard Masters ameziandikia klabu akitaka wachezaji wote wachanjwe na kusisitiza umuhimu wa kumalizika kwa msimu wa Ligi.

Nae meneja wa Brentford Thomas Frank alikuwa wa kwanza kutoa wito wa kusitishwa kwa mechi zote hadi tarehe 26 Disemba ili kuwezesha kupangwa kwa mpango mpya.

Baadhi wanahisi mapumziko yanapaswa kuwa marefu zaidi -lakini wengine kama Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp hawaamini hilo linapaswa kufanyika.

Primia Ligi ilisema Alhamisi kwamba inalengo la kuendelea kucheza mechi ili mradi ni salama kufanya hivyo.

Wakati huo huo, meneja wa , Manchester City Pep Guardiola ameruhusiwa kufufua maandalizi kwa ajili ya safari ya kuelekea Newcastle.

Muhispania huyo alilirejesha kipimo cha virusi vya corona ambacho hakikuwa kimekamilika na kuahirisha mkutano wa Ijumaa aliopanga kuufanya na waandishi wa habari, lakini kipimo cha haraka cha Covid PCR kiliporudi matokeo yalikuwa ni hasi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live