Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coutinho avigonganisha vilabu Ulaya

Skysports Philippe Coutinho 5695364 Philipe Coutinho

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi zinasema, Arsenal inamtaka Philippe Coutinho,29 kutoka Barcelona msimu huu wa majira ya joto kama hatajiunga moja kwa moja katika kikosi cha Aston Villa.

Tetesi zinasema, Erling Braut Haaland anatarajia kujiunga na Real Madrid au Barcelona, licha ya ripoti za mwishoni mwa wiki kudai kwamba mshambuliaji huyo amekubali mpango wa kujiunga na Manchester City.

Barcelona wanataka kumsajili moja kwa moja winga wà Hispania anayecheza klabuni hapo kwa mkopo Adama Traore, 26, kutoka Wolves katika dirisha la kiangazi na wanaweza kumtoa kiungo mhispania Riqui Puig, 22, kufanikisha mpango huo.

Tetesi zinasema, Winga wa Argentina Angel di Maria, 33, ameamua kwamba anataka kuondoka Paris St-Germain msimu huu na anaweza kurejea Benfica.

Kocha Mauricio Pochettino na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, ni miongoni mwa majina makubwa yatakayoondoka Paris St-Germain msimu huu.

Zinedine Zidane anatajwa huenda akamrithi Pochettino kama kocha wa PSG na tayari ameanza kuangalia wa kuwasajili kutoka klabu yake ya zamani ya Real Madrid, akiwemo kiungo Mbarazil Casemiro, 30.

Arturo Vidal, 34 anajiandaa kutimka Inter Milan msimu huu, huku klabu ya Flamengo ikionyesha nia ya kumrejesha Amerika Kusini kiungo huyo wa Chile.

Tetesi zinasema, Juventus iko tayari kumuuza kiungo mfaransa Adrien Rabiot, 26, msimu huu.

Roma wanajiandaa kupeleka ofa msimu huu kwa ajili ya mlinzi wa pembeni wa Barcelona mmarekani Sergino Dest, 21.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live