Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coutinho, Umtiti waiwekea ngumu Barca

Samuel Umtiti And Philippe Coutinho Philippe Coutinho na Samuel Umtiti

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Samuel Umtiti na Philippe Coutinho wanaripotiwa kuwa wamegoma kutoa sadaka mshahara wao kwa ajili ya kujihakikishia uhamisho wa kuondoka klabuni Barcelona.

Coutinho na Umtitii wamecheza mechi 13 pekee za La Liga msimu huu, na wote wamekuwa wakihusishwa na mipango ya kuondoka klabuni Barcelona, huku Countinho akitajwa kutaka kurejea Ligi Kuu ya Uingereza.

AC Milan pia wanaripotiwa kuwa wanahitaji huduma ya Umtiti, wakati Barca wakitajwa kuwa walijaribu kusitisha mkataba na staa huyu mara kadhaa. Mkataba wake wa sasa unaisha mwaka 2023.

kwa mujibu wa taarifa ya Spanish Reports, Barcelona wanapata waketi mgumu kuachana na Coutinho na Umtiti kwa sababu wawili hawa wapo tayari kuwa na mda mchache wa kucheza kwa malipo makubwa kuliko vinginevyo.

Mastaa hawa ni miungoni mwa wachezaji wanaolipwa vyema zaidi. Coutinho akilipwa Euro milioni 22 (Pauni milioni18.5) na Umtiti akilipwa Euro 16 (Pauni milioni 13.4) kila mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live