Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cosmopolitan mpo! Hebu wasikieni hawa wajeda

Cosmopolitan Tzzzz Cosmopolitan mpo! Hebu wasikieni hawa wajeda

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Rhino Rangers ikijiandaa kuwakabili Cosmopolitan kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), kocha wa timu hiyo, Athumani Bilali ‘Bilo’ amesema anawajua vizuri wapinzani wao na wala hana presha katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye uwanja wa Uhuru Desemba 14.

Msimu uliopita Rhino Rangers yenye maskani yake mjini Tabora iliishia hatua ya 16 bora ambapo ilitolewa na Yanga kwa kichapo cha mabao 7-0 katika pambano lililopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Rhino Rangers ambayo inashiriki First League itakutana na Cosmopolitan iliyoko Ligi ya Championship katika pambano hilo la hatua ya 64 bora ya mashindano hayo kusaka tiketi ya kufuzu raundi ya tatu.

Bilo amesema kikosi chake kipo sawa kuwakabili Cosmopolitan katika mchezo huo ambao kwao wanahitaji sana ushindi ambao utawapeleka katika hatua ya 32 bora hivyo wamejipanga vizuri kukabiliana na timu hiyo.

Amesema aliwaona wapinzani wao katika mechi mbili walizocheza na Pamba na Copco FC jijini Mwanza hivyo anajua mapungufu yao na eneo lipi la kuwakabili na kupata ushindi katika pambano hilo.

“Tutaanza safari yetu ya kwenda Dar es salaam Desemba 12, ni mchezo ambao kwetu tutahitaji sana ushindi uzuri kikosi changu kipo sawa na uzuri nimewaona Cosmopolitan hivyo tunajua jinsi ya kukabiliana nao na kupata ushindi,” amesema Bilo na kuongeza;

“Kikubwa tutacheza kwa umakini mkubwa ni lazima tuwaheshimu ni timu iliyotuzidi daraja na pia ina timu nzuri, nishawaambia wachezaji umuhimu wa huu mchezo hivyo tunahitaji kukaza,”

Chanzo: Mwanaspoti