Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Conte kutowapa mapumziko Mastaa waliokuwa Kombe la Dunia

Antonio Conte Sajili Kocha wa Spurs, Antonio Conte

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte amesema sio rahisi kuwapumzisha mastaa wake 12 waliotoka kwenye michuano ya kombe la dunia hivi karibuni.

Kikosi cha Tottenha kitamenyana na klabu ya Brentford siku ya jumanne huku ikiwa ni siku nane tu baada ya wachezaji wake wawili kucheza mchezo wa fainali ya kombe la dunia ambao ni nahodha Hugo Lloris na beki Christian Romero, Lloris anatarajiwa kua kwenye benchi siku ya jumanne huku Romero hatakuepo kwenye kikosi.

Kocha wa klabu hiyo Antonio Conte amesema kua itakua ngumu kwa yeye kuwapa muda mrefu wa kupumzika mastaa wake waliotoka kwenye michuano hiyo, kwasababu ya watakosa utimamu wa mwili kulingana na michezo ambayo inawakabili hapo mbeleni.

Lakini kocha huyo amefurahishwa na namna klabu yake ilivyofanikiwa kutoa wachezaji 12 kwenye michuano ya kombe la dunia, Akieleza kulingana na idadi hiyo inaonesha wako kwenye njia sahihi ambayo inaonesha wako kiushindani na wanaweza kushinda kitu.

Antonio Conte amesema wachezaji aliokua nao kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao hawakushiriki michuano ya kombe la dunia wana utimamu wa kimwili tofauti wale walioshiriki, Hivo jambo hilo linamfanya asiwape mda mrefu wa kupumzika wachezaji wake hao ili waweze kurudisha utimamu wa mwili mapema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live