Thu, 11 Nov 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kocha mpya wa Tottenham Antonio Conte amewazuia wachezaji wake kutumia “Mayonaizi” na ‘Sauce’ kwenye chakula kwa ajili ya kupambana na kuongezeka uzito.
Hii imekuja baada ya kocha huyo kugundua baadhi ya wachezaji wameongezeka uzito, na hivyo kuwataka wapunguze.
Conte pia ameagiza wachezaji wapungiziwe kiasi cha juisi ya matunda wanachopewa, na kuwataka wale zaidi matunda.
Muitalia huyo pia amewaagiza wapishi katika Kantini ya Spurs,kupunguza matumizi ya mafuta na siagi kwenye upishi wa vyakula vya wachezaji.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live