Kocha wa Tottenham Hotspur, Antonio Conte amempigia simu nyota wake, Harry Kane na kumpongeza mshambuliaji huyo kwa kuwa Mfungaji Bora wa muda wote wa klabu hiyo kwa goli lake la ushindi 1-0 dhidi ya Manchester City Usiku wa jana.
”Unanifanya nijivunie,” Conte amesikika kwenye simu aliyokuwa akiongea na Harry Kane.
Kocha huyo wa Tottenham alishindwa kuwasili uwanjani kwenye mchezo huo kutokana na kufanyiwa upasuaji nchini Itali na kikosi kiliongozwa na kocha msaidizi, Cristian Stellini.
Bao la Kane kipindi cha kwanza lilimfanya nahodha huyo wa England kufikisha mabao 267 kwa Spurs, na kuvunja rekodi iliyowekwa na marehemu Jimmy Greaves.