Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Conte ampendekeza Lukaku SSC Napoli

Lukaku Awatupia Mpira Chelsea Baada Ya Swali Kuhusu Klabu Ya Uingereza Conte ampendekeza Lukaku SSC Napoli

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu Mpya wa SSC Napoli Antonio Conte anajipanga kumsajili Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku kutoka Chelsea.

Lukaku amekuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya AS Roma msimu wa 2023/34 na Kocha Conte anaweza kumsajili kama mbadala wa Victor Osimhen.

Gazeti la The Evening Standard limeripoti kuwa, Conte amedhamiria kumsajili Lukaku baada ya kuwasilisha pendekezo hilo kwa viongozi wa juu wa SSC Napoli, ambao wanataka kuona klabu yao inarejesha heshima ya ubingwa msimu ujao.

Osimhen anatarajiwa kuondoka SSC Napoli msimu huu wa joto, akihusishwa na klabu ya Chelsea.

Hata hivyo klabu hiyo ya jijini London inakabiliwa na changamoto ya kumsajili Mshambuliaji huyo kutoka nchini Nigeria, kwa mujibu wa kifungu cha pauni milioni 113.

Chelsea huenda ikashindwa kutoa kiasi hicho cha pesa, hali ambayo inaweza kuleta ushindani dhidi ya klabu nyingine ambazo zitahitaji huduma ya Osimhen.

Ikumbukwe kuwa Antonio Conte aliwahi kufanya kazi na Lukaku alipokuwa akihudumu Inter Milan kama Mkuu wa Benchi la Ufundi mwaka 2019 hadi 2021.

Chanzo: Mwanaspoti