Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Conte aendeleza rekodi Tottehnam ikiichapa Brentford

Son Heung Min 1hinko9rlq6b21jt8oshj13zav.jpeg Tottenham yaichapa Brentford

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Antonio Conte ameendeleza rekodi ya kutopoteza mechi ligi Kuu tangu aliposhika majukumu ya kukinoa kikosi hicho baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Brentford.

Goli la kujifunga la Sergio Canos na Heung-min Son, yameipa ushindi Tottenham unaomfanya Conte kufikisha ushindi wake wa pili mfululizo.

Tangu kuwasili kwa Antonio Conte aliyechukua mikoba ya Nuno Santo aliyetimuliwa kutokana na matokeo mabovu kikosini hapo.

Conte ameshinda dhidi ya Leeds, Brentford na sare dhidi ya Everton. Mchezo dhidi ya Burnley uliahirishwa siku ya Jumapili kutokana na uwanja kujaa barafu.

Kwa ushindi huo, Tottenham imefikisha alama 22 na kusogea mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa EPL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live