Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Conte: Kikao na EPL Ilikuwa ni Kupoteza Muda Tu

Antonio Conte Sp.jpeg Antonio Conte

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Tottenham Antonio Conte amesema kwamba kikao cha Premier League na makocha wa vilabu vya ligi hiyo kuhusu upangaji ratiba ilikuwa ni kupoteza muda tu.

Walimu wa timu za Ligi kuu walikutana siku ya Alhamisi kuelezea wasiwasi wao juu ya ustawi wa wachezaji kutokana na mahitaji waliyowekewa wakati wa sikukuu zenye mambo mengi.

Milipuko ya Virusi vya Corona kwenye vilabu imesababisha michezo mingi kuahirishwa hivi majuzi, huku baadhi ya mechi zikiendelea.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola alipendekeza wachezaji wanaweza kufikiria kugoma ili kuleta mabadiliko.

Kocha mkuu wa Tottenham Conte haamini kuwa lolote lilipatikana katika mkutano na Premier League.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live