Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Congo yasitisha shuhguli zote za michezo viwanja vya Kinshasa

Kinshasa 13 Congo yasitisha shuhguli zote za michezo viwanja vya Kinshasa

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shughuli zisizo za michezo zimesitishwa katika Viwanja vya Martyrs na Tata Raphael huko Kinshasa,” ametangaza Jacquemain Shabani, Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani.

Mamlaka ya DR Congo imechukua uamuzi huu siku ya Jumapili kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea siku moja kabla katika uwanja wa Martyrs wakati wa tamasha la Injili.

Takriban watu saba walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya Jumamosi jioni katika mkanyagano wakati wa tamasha la hilo katika uwanja wa michezo wa Stade des Martyrs wenye uwezo wa kubeba Mashabiki 80,000.

Mkanyagano huo ulitokea Jumamosi wakati wa tamasha la msanii Mike Kalambayi, mwanamuziki maarufu wa Injili wa DR Congo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, mkasa huu ulisababisha vifo vya watu 8 na kuacha majeruhi kadhaa.

Bw. Shabani anasema tayari uchunguzi unaendelea ili kubaini makosa ya jinai na kiraia kwa tukio hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live