Rais wa DR Congo, H.E Félix-Antoine Tshisekedi ametangaza nia ya kuandaa Kombe la Mataifa huru ya Afrika 'AFCON' 2029, likiwa ni kulitangaza taifa hilo lenye utajiri wa madini.
DRC ni mmoja wa washiriki wakuu wa AFCON, akiwa ameshiriki mara 19 katika misimu 34 ya AFCON .Pia ni moja ya timu zilizofanikiwa zaidi barani Afrika, ikiwa imeshinda mataji mara mbili mnamo 1968 na 1974, huku wakicheza nusu fainal mara 3, mnamo 1998 ,2015 na 2023
DRC haijawahi kuandaa mashindano hayo kabla, ikiwa ombi lao litakubaliwa basi itakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mashindano kubwa zaidi ya ya mpira barani Afrika.