Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Colwill apewa maua yake Chelsea

Levi Colwill Colwill apewa maua yake Chelsea

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki Levi Colwill wa Chelsea amemwagiwa sifa kufuatia kiwango bora alichokionyesha katika ushindi wa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Fulham, wakiwemo wachezaji wenzake Cole Palmer na Ian Maatsen.

Chelsea walipata ushindi muhimu wakiwa ugenini kwa kuwachapa Fulham mabao 2-0 kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu England.

Mykhailo Mudryk na Armando Broja wote walifunga mabao katika kipindi cha kwanza na kuifanya timu hiyo kupata ushindi wake wa pili kwenye ligi baada ya michezo saba.

Levi Colwill aliposti kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram mara baada ya ushindi huo, akionyesha alivyofurahia matokeo hayo muhimu kulingana na namna walivyouanza msimu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, alitoa pasi ya bao la kwanza kwa Mudryk.

Cole Palmer alitoa maoni yake akimsifia kwa upande wake, Mudryk alisema,"Bonge la mchezaji."

Wakati huohuo, mchezaji wa akiba wa Chelsea Ian Maatsen naye alifurahishwa na uchezaji wa Colwill kwa kutumia ishara ya moto.

Sasa, vijana hao wa Mauricio Pochettino watasafiri kwenda Burnley wikendi hii kwa mchezo wao wa mwisho kabla ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.

Chanzo: Mwanaspoti