Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Colombia wanatisha nyie!, hakuna wakuwazuia

Babake Luis Aachiliwa Na Waasi Wa Colombia Colombia wanatisha nyie!, hakuna wakuwazuia

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Colombia imetinga fainali ya michuano ya Copa America kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa zaidi ya miongo miwili.

Colombia wamesubiri kwa miaka 23 ili kucheza tena fainali ya Copa America ambapo mara ya mwisho walicheza mwaka 2001 walipoifunga Mexico na kutwaa ubingwa wao wa kwanza na wa kipekee katika michuano hiyo.

Alfajiri ya leo Colombia wameifunga Uruguay bao 1-0 na watakutana na mabingwa watetezi Argentina kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa Julai 15.

Katika hatua nyingine wababe hao wa kandanda kutoka America Kusini wameendelea kutuma ujumbe mzito ulimwenguni kwa kuendeleza rekodi ya kutopoteza kwenye michezo 28 waliyocheza.

Kwa sasa Colombia inatazamwa kama moja ya timu tishio zaidi ulimwenguni kutokana na ubora wanaonesha wakiongozwa na nahodha James Rodrigues ambaye amekuwa kiungo muhimu katika ushindi wa timu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live