Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cody Gakpo anafaa kuwa mbadala wa Cristiano Ronaldo

Coady Gapko Holland Coady Gapko

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag anaonekana kuwasha taa za kijani katika juhudi za kumnasa Cody Gakpo kutoka PSV Eindhoven.

Ushindani unatarajiwa kuwa mkali kwa Mholanzi huyo baada ya kuonesha kiwango kikubwa kwenye Michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, na anaweza kuwasili Old Trafford Januari kama mbadala wa Cristiano Ronaldo.

Uongozi wa Mashetani Wekundu unafahamu ugumu wa kufanya usajili dirisha la Januari baada ya Ten Hag kufanya matumizi makubwa ya uhamisho wakati wa majira ya joto.

Hata hivyo, kuondoka kwa Ronaldo kumeacha pengo kubwa kwenye kikosi hicho ambalo ni lazima lijazwe ili kuipa United nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi nne za juu.

Ten Hag alitanguliza usajili wa Antony badala ya Gakpo msimu wa joto lakini anaweza kurejea kwa mara ya pili kwenye njia hiyo baada ya Mwaka Mpya.

Fowadi huyo wa PSV amegeuka na kuwa mashine ya mabao na kusaidia katika msimu wa 2022/23 na vilabu vingi vya juu vinajiandaa kuinasa saini yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live