Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Cody Gakpo Asisitiza Kuwa Liverpool ina Mengi ya Kuboresha

Gakpo Header Cody Gakpo

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cody Gakpo amesisitiza kuwa timu yake mpya ya Liverpool ina mengi ya kufanya na kuboresha zaidi baada ya kutoa sare ya 2-2 Jumamosi jioni dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika raundi ya tatu ya Kombe la FA.

Timu hizo mbili za Premier League watahitaji dakika 90 zaidi, pamoja na uwezekano wa muda wa ziada na penati, Januari 28 ili kuwatenganisha baada ya sare hiyo pale kwenye dimba la Anfield.

Goncalo Guedes aliwapatia Wolves bao la kuongoza la mapema baada ya makosa mabaya ya Alisson Becker, lakini mabao ya Darwin Nunez na Mohamed Salah yaligeuza ubao.

Mabadiliko ya kipindi cha pili kutoka kwa Julen Lopetegui kwa mara nyingine yaliipa timu yake msukumo, Matheus Cunha na Hwang Hee-Chan wakitokea benchi na kufunga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliocheza mechi yake ya kwanza baada ya kusajiliwa kwa takriban paundi milioni 40 wiki iliyopita na alionekana kama mshambuliaji hatari zaidi wa Liverpool.

Mchezo mzuri wa mchanganyiko kati yake, Andy Robertson, na Thiago Alcantara ulitoa faraja kuhusu jinsi watatu hao wataungana katika siku zijazo.

“[Ilikuwa] hali nzuri sana,” Gakpo aliiambia Liverpoolfc.com. “Kwa mchezo wangu mwenyewe, nadhani nilionyesha wakati mzuri na wakati wa kizembe. Kwa hivyo, bado ninaweza kuboresha sehemu hizo na kuendelea kufanya kazi na kujaribu kusaidia timu kadri niwezavyo.

“Bila shaka, unajifunza zaidi unapocheza michezo, kwa hivyo ninatazamia [zaidi].

“Nadhani tulicheza kwa awamu mpira mzuri sana lakini mwishowe, hatukupata bao la kutosha, kwa hiyo ni jambo la kusikitisha. Lakini nadhani tulionyesha tunachoweza kufanya lakini bado tunaweza kuboresha baadhi ya maeneo”

“Nadhani tulionyesha ari ya timu kwa wakati fulani, kwa hivyo hiyo ni nzuri. Nadhani tunapaswa kwenda huko [Molineux] kwa dhamira kubwa na kwenda tu kupata ushindi.”

Liverpool wana muda mwingi wa kupumzika kabla ya kurejea Ligi Kuu wikendi ijayo kutokana na kuondolewa kwenye Kombe la Carabao. Lakini kwa kuwa Wolves wamepangiwa mpambano wa robo fainali siku ya Jumatano, huenda mchezo wowote wa marudiano ukafanyika wiki inayoanza Januari 16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live