Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal yaigomea Yanga mapema

Mashabiki Coastal Union Coastal yaigomea Yanga mapema

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baadhi ya mashabiki wa Yanga wanaamini Coastal Union imeingia pabaya kupangwa kukutana na timu yao katika fainali ya ASFC, lakini Wagosi wameibuka na kupiga mkwara wakisema vinara hao wa Ligi Kuu Bara wasitarajie mteremko kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Yanga na Coastal zinatarajia kuvaana katika mechi ya fainali ya michuano hiyo itakayopigwa Julai 2 kuwania taji lililotemwa na Simba iliyokuwa ikilishikilia kwa misimu miwili mfululizo baada ya kila mmoja kushinda mechi zao za nusu fainali dhidi ya Simba na Azam.

Yanga iliifunga Simba kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na Coastal kuiondosha Azam kwa mikwaju ya penalti 6-5 baada ya dakika 120 kumalizika kwa suluhu.

Timu hizo zitakutana pia katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara ambapo kama Yanga itashionda itatangaza ubingwa wakiipokea Simba na Wagosi wametamka kwamba hawapo tayari kugeuza daraja la kuwapa vijana wa Jangwani mataji mawili kirahisi kama wanavyofikiria.

Nahodha Msaidizi wa Coastal, Aman Kyata aliliambia Mwanaspoti kuwa, wanajua Yanga inataka kutangaza ubingwa wa ASFC na Ligi Kuu kupitia kwao, ila hawatakubali kwani wao wanafikiria zaidi kumaliza ligi ndani ya nafasi nne za juu na pia kukatav tiketio ya michuano ya CAF.

“Ngoja tuone ila sisi tutapambana kupata pointi tatu kwani tunataka msimu huu tumalize ndani ya nne bora. Ukiangalia kwa sasa tuko nafasi ya sita hivyo kama tutakomaa na kupata matokeo mazuri kwenye mechi hizo nne basi lazima malengo yetu ya kumaliza ndani ya nne bora yatimie.

“Tunajua Yanga ni timu nzuri na inajiandaa kuhakikisha pengine inatangazia ubingwa kwetu lakini sisi tunajiandaa pia kwani tunataka pointi tatu au tukishindwa basi hata moja,” alisema Kyata.

Kuhusu mchezo wa fainali ya ASFC, Kyata alisema itakuwa moja ya mechi nzuri kwani anamini Yanga tayari watakuwa mabingwa na wao watakuwa hawana cha kupoteza zaidi ya kuutaka ubingwa katika mchezo huo.

“Ile ni fainali na tumestahili kuwa hapa tulipofika kwani tumezitoa timu nyingi. Uzuri wa fainali ni kwamba hakuna mtu atakayemdharau mwenzake kwani kila mmoja anatafuta ubingwa,” alisema Kyata.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz