Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal wazidi kutakata Ligi Kuu, wakwea nafasi ya Tisa

Sopu A Goal 2 Mfungaji wa Magoli ya Coastal Union, Abdul Suleiman ‘Sopu’

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Coastal Union wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchezo uliopigwa jana Ijumaa katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Mabao ya Coastal yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ yote mawili dakika ya saba na 15, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Anuary Jabir dakika ya 23.

Coastal Union wanafikisha pointi 31 na kusogea nafasi ya tisa, huku Dodoma Jiji ikibaki na pointi zake 28 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 25

Chanzo: www.tanzaniaweb.live