Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal watuma salamu Dodoma Jiji

Coastal Union Kikosi Geita Coastal watuma salamu Dodoma Jiji

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Coastal Union ’Wagosi wa Kaya’ wametamba kuwaharibia sherehe ya Pasaka mashabiki wa timu ya Dodoma Jiji kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kufanyika saa moja jioni katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Timu hiyo inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 26 huku Dodoma Jiji ikishika nafasi ya 11 ikiwa na alama 27,timu zote zimecheza michezo 25.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga,Dodoma Jiji iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Rashid Chambo kwa shuti kali.

Chambo msimu uliopita aliichezea Coastal Union lakini msimu huu alisajiliwa na kocha Masoud Djuma ambaye alitupiwa virago na nafasi yake ilichukuliwa na Melis Medo ambaye yupo na timu hiyo mpaka sasa.

Kocha wa timu hiyo,Fikiri Elius amesema wataingia kwa tahadhari katika mchezo huo kutokana na ubora wa Dodoma Jiji huku akidai wamejipanga kuondoka na alama tatu.

“Tumejiandaa vizuri mechi ya Dodoma na Coastal huwa na changamoto zake, tutegemee utakuwa mchezo mzuri.Kusimama kwa mechi imekuwa faida tumepata muda wa kurekebisha katika kuijenga vizuri timu yetu,”amesema Kocha huyo.

Nahodha wa timu hiyo,Felly Mulumba amesema : “ Sisi tupo tayari kwa mechi yetu ya kesho,”.

Kwa upande wake Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji,Kassim Liogope amesema michezo ya kirafiki waliyocheza na timu za Ligi Kuu,Mbeya City,Kagera Sugar na Singida Big Stars imewasaidia kujua mapungufu yao yapo wapi.

“Kwanza tunapenda kuishukuru Menejiment yetu kwa kututafutia michezo ya kirafiki ambayo imetupa kipimo sahihi,tupo tayari kwa mchezo huo na asilimia 99 ya wachezaji wetu watakuwepo,”amesema Kocha huyo.

Nahodha wa timu hiyo,Mbwana Kibacha amesema “Sisi tumejiandaa vizuri morali ipo juu tumepata muda wa kutosha katika kipindi ambacho tumefanya mazoezi ni hichi tumecheza mechi za kueleweka imani yetu tutashinda na hilo linawezekana,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live