Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal waivuruga Prisons Uwanja wa Sokoine

Prisons Vs Coastal Coastal waivuruga Prisons Uwanja wa Sokoine

Thu, 10 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Coastal Union imetafuna vyema kipolo chake kwa kuikandika Tanzania Prisons mabao 2-0 na kumaliza vyema dakika 90 za mchezo wake wa Ligi Kuu uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini hapa na hizi ni dondoo za mechi hiyo.

Coastal Union kabla ya mchezo wa leo ilikuwa timu pekee iliyokuwa imecheza mechi chache (saba) kuliko timu yoyote Ligi Kuu ikiwa imekusanya pointi nane na kukaa nafasi ya 12.

Katika dakika 45 za kwanza Wagosi hao walikuwa bora sana kuliko wenyeji Prisons kutokana na kupata nafasi nyingi lakini zaidi wakipata kona tisa kwa japokuwa hazikuwa na faida kwao kufunga mabao, huku Prisons wakipata tatu hadi dakika 90 za mchezo.

Kutokana na kuutawala mpira kwa kipindi cha kwanza walitumia vyema nafasi moja kupata bao dakika ya nne kupitia kwa Straika wake Maabad Maulid aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Moubarack Amza kabla ya Hamad Majimengi kuongeza la pili dakika ya 61.

Tanzania Prisons walionekana kutumia nguvu zaidi kulazimisha mashambulizi hali iliyowaathiri na kufanya wachezaji wake wawili, Joshua Nyantin na Dotto Shaban na Michael Masinda kuoneshwa kadi za njano kwa dakika ya 12, 35 na 72 na mwamuzi Ally Mnyupe kutoka Morogoro.

Prisons iliwapumzisha Jumanne Elfadhir, Samson Mbangula, Jeremiah Juma na Zabona Hamis na Hamis Mcha na kuwaingiza Benjamin Asukile, Michael Ismail, Mudathir Said, Ismail Mgunda na Marco Mhilu dakika ya 68 na 81.

Kipa wa Coastal Union alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kujazwa na Mohamed Hussein, huku Maabad akimpisha William Kisingi dakika ya 83 na Majimengi akimuachia nafasi Gustafa Simon mabadiliko hayo yaliipa uhai Coastal Union kuendelea kumiliki mpira kuliko wenyeji wa mpambano huo.

Hata hivyo katika mchezo huo ilishuhudiwa wakikutana kwa mara ya kwanza makocha Patrick Odhiambo (Prisons) na Yusuph Chipo wa Coastal Union ambao wote ni raia wa Kenya.

Mechi hiyo ilikuwa ni kiporo ambapo awali timu hizo zilikuwa zikutane Oktoba 17, lakini Coastal Union waliomba kusogezwa mbele kufuatia wachezaji wake watatu kuwa katika majukumu na timu ya Taifa ya vijana (U23) na sasa itsalia kwenye uwanja wa Sokoine kumenyana na Mbeya City, Novemba 13 kumaliza vipolo vyake.

Chanzo: Mwanaspoti