Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal waichapa Ihefu Mkwakwani

Coastal Vs Ihefu Mkwakwani Coastal waichapa Ihefu Mkwakwani

Sun, 14 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Coastal Union ikiwa nyumbani imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ihefu na kujiweka katika mazingira salama zaidi nafasi ya 9 kwenye msimamo wakijitoa katika eneo la hatari ya kushuka daraja msimu huu.

Bao pekee katika mchezo huo limewekwa wavuni na Moubrack Amza dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza.

Coastal Union wamekuwa na mwendelezo mzuri hivi karibuni ikiwa katika michezo yao mitano iliyopita wameshinda mitatu na kutoa sare michezo miwili.

Ihef wamekuwa na mwendelezo wa matokeo mabovu kwa siku za hivi karibuni baada ya kupoteza michezo yao mitatu mfurulizo wakishika nafasi ya 8 kwenye msimamo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: