Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal vs Yanga ni heshima tu Mkwakwani leo

Yanga Vs Coastal Final.jpeg Coastal vs Yanga ni heshima tu Mkwakwani leo

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchi la ufundi la Coasta Unio limesema kuwa timu hiyo itacheza kwa heshima na nidhamu kubwa leo dhidi ya Yanga kwenye mechi ya Ligi Kuu katika Uwanja wa Mkwakwani kuanzia saa 12:30 jioni kutokana na ubora wa wapinzani wao.

Kwa mujibu wa rekodi, miongoni mwa viwanja vigumu kwa Yanga ni pamoja na CCM Mkwakwani, Tanga kwani kwenye michezo sita ya mwisho kucheza kwenye uwanja huo dhidi ya wagosi hao wa kaya, wameshinda mara mbili, kupoteza nako ni mara mbili huku wakitoka sare pia mara mbili.

Licha ya ugumu huo ndani ya misimu miwili iliyopita, Yanga imeshinda mfululizo kwa mabao 2-0 kwenye kila mchezo huku aliyekuwa mshambuliaji wa kikosi hicho, Fiston Mayele akifunga bao moja kwenye kila mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: