Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal union inataka tiketi ya CAF

Coastal Vs Mtibwa.jpeg Coastal union inataka tiketi ya CAF

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Coastal Union, Ley Matampi amesema mabeki wa timu hiyo ni sababu ya yeye kufanya vizuri kutokana na hatari nyingi kuishia miguuni mwao huku akiitabiria timu hiyo nafasi nne za juu.

Matampi, raia wa DR Congo ameonekana kuwa chaguo la kocha David Ouma ambaye tangu ametua msimu huu, amecheza mechi 10 akiruhusu mabao manne tu.

Hadi sasa Matampi ndiye kinara ambaye hajaruhusu wavu wake kugusa katika mechi saba kwenye Ligi Kuu Bara akiwaacha Yona Amos (Prisons) mwenye sita, Djigui Diara wa Yanga aliye na tano sawa na Constantine Malimi (Geita Gold) na John Noble wa Tabora United.

Akizungumza na Mwanaspoti, Matampi ambaye amewahi kuhusishwa na Simba na Yanga miaka mitano iliyopita,alisema mipira ambayo muda mwingine huonekana hatari huishia miguuni mwao akieleza kuwa wametengeneza muunganiko mzuri ambao unaipa matokeo mazuri timu hiyo.

“Najivunia kiwango bora licha ya muda mfupi niliotua Tanzania, lakini siwezi kutowapongeza mabeki kutokana na kazi nzuri wanayofanya, ipo mipira ya hatari wanaizuia.

“Hii kwangu ni mara ya kwanza kuwa kinara wa ‘cleen sheet’ katika Ligi Kuu, inaonyesha ubora lakini lazima niendelee kupambana na kujihakikishia nafasi zaidi kikosini,” alisema kipa huyo.

Nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa DR Congo, aliongeza kwamba kutokana na msimu bora alionao anatamani kwamba atabeba tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu na pia kuiweka timu yake nafasi ya nne.

Chanzo: Mwanaspoti