Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal kutibua rekodi ya Azam

Coastal Pix Coastal kutibua rekodi ya Azam

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kufungwa michezo miwili mfululizo Kocha wa Coastal Union, Yusuf Chippo amesema wiki moja kwao imetosha kurekebisha kasoro zilizojitokeza hivyo matokeo hayo hayajawatoa wachezaji wake kwenye njia na kwamba watapata matokeo dhidi ya Azam inayojinasibu kutopoteza mechi.

Coastal inacheza na Azam FC Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex huku timu hizo zikitoka suluhu mara ya mwisho zilipokutana Machi Mosi mwaka huu.

Hata hivyo ‘Wagosi wa Kaya’ watakuwa na kazi kubwa ya kuizuia Azam kwani tangu timu hiyo amekabidhiwa Kally Ongala haijawahi kufungwa wala kutoa sare, katika michezo sita aliyokiongoza ameshinda yote.

Coastal ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mtibwa Sugar na Ihefu huku Chippo akiweka wazi ishu kubwa inayoendelea kuwaangusha ni washambuliaji wake kushindwa kutumia vizuri nafasi zinazopatikana.

“Ni kweli tunafunga na wachezaji wangu wanajitahidi ila bado wanakosa nafasi nyingi ambazo tungeweza kufunga mabao zaidi, ni tatito ambalo tunaendelea kulirekebisha na kulipa uzito,” alisema na kuongeza;

“Mechi zimekuwa karibu karibu na hata maandalizi yenyewe yanakuwa kwa muda mchache, akili zetu ni kwa Azam tukitambua tunaenda kucheza na timu imara japo tunahitaji kurudisha furaha kwa mashabiki zetu,”alisema.

Mshambuliaji wa Coastal, Hamad Majimengi alisema ugumu wa ligi ndio chanzo cha wao kuwa na matokeo mchanyanyiko ingawa wanajiamini.

Chanzo: Mwanaspoti