Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal kumaliza hasira kwa Dodoma Jiji

Coastal Union FCC Kikosi cha Coastal Union

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Azam, klabu ya Coastal union wanatarajia kumkaribisha Dodoma Jiji katika mchezo wao wa ligi kuu ya NBC leo katika uwanja wa Mkwakwani.

Coastal ambao juzi hapo wamefanya tukio la kumvamia mwamuzi kutokana na muda ambao uliongezwa lakini kutokana na kupoteza kwao muda na mwamuzi hakumaliza mechi mpaka zikafika dakika 101.

Timu hiyo ya mkoani Tanga wapo nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi 12 wakiwa wameshinda mechi tatu pekee, wakienda sare mara tatu lakini pia wakiwa wamepoteza michezo sita pointi 12 kileleni.

Wakati Dodoma Jiji wao wapo nafasi ya 15 baada ya kucheza mechi 13 ushindi mara mbili, sare tatu na wamepoteza michezo nane huku wakijivunia pointi zao tisa kwenye msimamo mpaka sasa.

Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili Wagosi wa kaya waliondoka na pointi tatu muhimu. Mchezo wa kesho utakuwa muhimu kwa kila timu kwani timu zote hizo haziko kwenye nafasi nzuri hasa Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live